Duration 2:57

TAZAMA,, WANANCHI WAMLILIA MAGUFULI, TUNABAKWA, TUMEPORWA MASHAMBA YETU HATUNA PAKULIMA.

157 watched
0
1
Published 9 Nov 2021

UVINZA-KIGOMA. WANANCHI katika Kata ya Ilagara wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamelazimika kusitisha shughuli za kilimo kutokana na kukosa maeneo ya kulima, baada ya maeneo waliyokuwa wakilima awali kudaiwa kuchukuliwa na Jeshi la Magereza huku wengine wakidai kunyanganywa mazao na kuchomewa moto nyumba zao ili kupisha maeneo hayo. Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mheshimiwa samia suluhu hassani awasaidie kuendelea kulima katika maeneo hayo ambayo wamekuwa wakilima kwa miaka mingi. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Uvinza Hanafi Msabaha amesema tayari zaidi ya ekari elfu moja mia sita zimetolewa kwa wananchi hao baada ya mgogoro na kwamba kama eneo hilo bado halikidhi mahitaji yao watafute maeneo katika vijiji vingine kwa kuwa maeneo waliyopewa jeshi la magereza yataendelea kumilikiwa na magereza. MWISHO.

Category

Show more

Comments - 0